Az-Zukhruf 43:21
الزخرفأَمْ ءَاتَيْنَـٰهُمْ كِتَـٰبًا مِّن قَبْلِهِۦ فَهُم بِهِۦ مُسْتَمْسِكُونَ
Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hiki, na ikawa wao wanakishikilia hicho.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hichi, na ikawa wao wanakishikilia hicho? [21]
[21] Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya Qur'ani cha kuunga mkono huu uzushi wao, ndio maana wakashikamana nao kwa nguvu hivi? Hatukuwateremshia Kitabu namna hiyo. Basi hawana hoja ya kuinukulu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, walishuhudia uumbaji wa Malaika au tuliwapatia kitabu kabla ya hii Qur’ani tuliyoiteremsha, wakawa wameshikamana nacho, na wanakifanyia kazi na wanajijengea kwa hicho hoja za kukupinga, ewe Mtume?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net