Az-Zukhruf 43:20
الزخرفوَقَالُوا۟ لَوْ شَآءَ ٱلرَّحْمَـٰنُ مَا عَبَدْنَـٰهُم ۗ مَّا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ
Nao husema: 'Angelipenda Mwingi wa Rehema tusingeliwaabudu sisi.' Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uongo tu!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nao husema: Angeli penda Mwingi wa Rehema tusingeli waabudu sisi. Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uwongo tu! [20]
[20] Na washirikina husema ati: Lau kuwa Mwingi wa Rehema angeli kuwa anataka tusiiabudu hii miungu basi tusingeli iabudu. Wanakusudia kudai kuwa ati Mwenyezi Mungu yu radhi kuabudiwa hiyo miungu. Wanasema hayo bila ya kuwa na ilimu yoyote ya kuyategemezea wayasemayo. Hawa si chochote ila ni wenye kudhani tu. Hunena maneno yasio na ushahidi wowote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawa washirikina wa kikureishi wanasema, Lau Allah Mtukufu Mwingi wa rehema angetaka tusingeabudu yoyote asiyekuwa Yeye.” Na hii ni hoja iliyotenguka, kwani Allah Mtukufu Ashasimamisha hoja juu ya waja kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu, basi kujisimamishia hoja ya Mapitisho na Makadirio ni ubatilifu mkubwa zaidi baada ya Mitume kuwaonya. Wao hawana ujuzi wa hakika ya yale wanayoyasema. Hakika ni kwamba wao wanayasema kwa kudhania na kuzua urongo, kwa kuwa hawana habari wala dalili kuhusu hilo kutoka kwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net