Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 18

Az-Zukhruf 43:18

الزخرف

أَوَمَن يُنَشَّؤُا۟ فِى ٱلْحِلْيَةِ وَهُوَ فِى ٱلْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ

Maana

Ati aliyelelewa katika mapambo na katika mabishano hawezi kusema kwa bayana?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ati aliye lelewa katika mapambo, na katika mabishano hawezi kusema kwa bayana? [18]

[18] Hivyo hawa wana fanya jeuri ya kumpachikia Mwenyezi Mungu mwana, ambaye kwa maumbile yake amelelewa katika mapambo, na hata hawezi kujadiliana na kupambana kwa hoja kwa nuksani yake ya kubaini. Ama hili ni jambo la ajabu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hivi mna ujasiri wa na kumnasibishia Allah Mtukufu mtu anayelelewa katika pambo, asiyeweza kubainisha hoja kwenye mjadala kwa sababu ya kukulia kwake kwenye pambo na starehe?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net