Az-Zukhruf 43:17
الزخرفوَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحْمَـٰنِ مَثَلًا ظَلَّ وَجْهُهُۥ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ
Na anapobashiriwa mmoja wao kwa yale aliyompigia mfano Mwenyezi Mungu, uso wake husawijika na hujaa hasira.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na anapo bashiriwa mmoja wao kwa yale aliyo mpigia mfano Mwenyezi Mungu, uso wake husawijika na hujaa hasira. [17]
[17] Wamekuzulia Wewe hayo, na ilhali wao akipewa khabari mmoja wao kwamba amepata mtoto wa kike uso wake husawajika kwa kuudhika, naye kajaa masikitiko na huzuni kwa kuona anapewa khabari mbaya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na anapopewa bishara mmoja wao ya mtoto wa kike ambaye amemnasibishia Mwingi wa rehema, alipodai kwamba Malaika ni watoto wa kike wa Allah Mtukufu, uso wake unageuka unakua mweusi kwa bishara mbaya aliyopewa ya mtoto wa kike, na huwa na huzuni na kujawa na simanzi na unguliko.(Basi vipi wataridhika kwa Allah Mtukufu kitu ambacho wao wenyewe hawaridhiki nacho? Ametukuka Allah Mtukufu kutukuka kukubwa na Ametakasika na kile wanachosema hao makafiri.)
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net