Az-Zukhruf 43:14
الزخرفوَإِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ
Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi. [14]
[14] Na hakika sisi ni wenye kurejea kwa Muumba wetu baada ya maisha haya, ili ahisabiwe kila mmoja kwa iliyo tanguliza mikono yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ili mseme pia, «Na sisi baada ya kufa kwetu ni wenye kuelekea Kwake na kurejea». Hapa pana dalili ya kuwa Allah Mtukufu Ndiye Mwenye kuwaneemesha waja Wake kwa neema mbalimbali, Ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa kwa kila hali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net