Az-Zukhruf 43:13
الزخرفلِتَسْتَوُۥا۟ عَلَىٰ ظُهُورِهِۦ ثُمَّ تَذْكُرُوا۟ نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا ٱسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا۟ سُبْحَـٰنَ ٱلَّذِى سَخَّرَ لَنَا هَـٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُۥ مُقْرِنِينَ
Ili mkae vizuri migongoni mwao, kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa sawa sawa juu yao, na mseme: 'Ametakasika aliyemfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya haya wenyewe.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ili mkae vizuri migongoni mwao, kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa sawa sawa juu yao na mseme: Ametakasika aliye mfanya huyu atutumikie, na tusingeli weza kufanya haya wenyewe. [13]
[13] Ili mtulie juu yao, kisha mkumbuke neema za Muumba wenu na Mlezi wenu kwa kuvifanya hivyo vikutumikieni mnapo tulia juu yao, na kwa kuadhimisha kule kuvifanya vinyonge kwa njia ya ajabu, na kutambua uweza mlio wezeshwa kuvidhibiti na kuvitawala, mseme: Subhana, Ametakasika aliye mfanya huyu (au hichi) kuwa dhalili kututumikia na sisi wenyewe tusingeli weza kumdhalilisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mpate kujituliza juu ya migongo ya hivyo mnavyovipanda, kisha mkumbuke neema ya Mola wenu kwenu hapo mnapopanda na mseme, «Sifa njema zote ni za Allah Mtukufu Aliyetudhalilishia (kipando) hiki, na hatukuwa ni wenye uwezo juu yake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net