Ash-Shura 42:17
الشورىٱللَّهُ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ ٱلْكِتَـٰبَ بِٱلْحَقِّ وَٱلْمِيزَانَ ۗ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ ٱلسَّاعَةَ قَرِيبٌ
Mwenyezi Mungu ndiye aliyeteremsha Kitabu kwa Haki na Mizani. Na ni nini kitakachokujulisha ya kwamba pengine Saa ya Kiyama ipo karibu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu ndiye aliye teremsha Kitabu kwa Haki, na Mizani. Na nini kitakacho kujuulisha ya kwamba pengine Saa ya Kiyama ipo karibu? [17]
[17] Mwenyezi Mungu ndiye aliye teremsha Kitabu cha Muhammad na viliyo kuwa kabla yake katika Vitabu vya Mitume, vyenye kukusanya Haki na uadilifu. Na nini cha kukujuvya, pengine wakati wa Saa ya Kiyama ipo karibu na wewe hujui.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Ndiye Aliyeteremsha Qur’ani na Vitabu vilivyoteremshwa vinginevyo kwa ukweli. Na Ameteremsha mizani, nayo ni uadilifu, ili Ahukumu baina ya watu kwa usawa. Na ni lipi linalokujulisha na kukufahamisha kuwa huenda wakati ambao Kiyama kitasimama uko karibu?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net