Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 16

Ash-Shura 42:16

الشورى

وَٱلَّذِينَ يُحَآجُّونَ فِى ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مَا ٱسْتُجِيبَ لَهُۥ حُجَّتُهُمْ دَاحِضَةٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ

Maana

Na wale wanaohojiana juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kukubaliwa, hoja za hawa ni batili mbele ya Mola wao Mlezi, na juu yao ipo ghadhabu, na itakuwa kwao adhabu kali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanao hojiana juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kukubaliwa, hoja za hawa ni baat'ili mbele ya Mola wao Mlezi, na juu yao ipo ghadhabu, na itakuwa kwao adhabu kali. [16]

[16] Na hao wanao bisha katika mambo yaliyo khusu Dini ya Mwenyezi Mungu, baada ya watu kwisha uitikia Wito ulio wazi, ubishani wa watu hawa wenye shaka shaka ni baat'ili mbele ya Mola wao Mlezi. Na juu yao ipo ghadhabu kali kwa ukafiri wao. Na adhabu chungu inawangojea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanaojadili kuhusu Dini ya Allah Mtukufu niliyomtuma kwayo Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), baada ya watu kuikubali na kusilimu, hoja zao na mijadala yao, mbele ya Mola wao, ni yenye kutenguka na kuondoka. Na watashtukiziwa na adhabu kutoka kwa Allah Mtukufu hapa duniani, na huko Akhera watakuwa na adhabu kali, nayo ni Moto.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net