Fussilat 41:50
فصلتوَلَئِنْ أَذَقْنَـٰهُ رَحْمَةً مِّنَّا مِنۢ بَعْدِ ضَرَّآءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ هَـٰذَا لِى وَمَآ أَظُنُّ ٱلسَّاعَةَ قَآئِمَةً وَلَئِن رُّجِعْتُ إِلَىٰ رَبِّىٓ إِنَّ لِى عِندَهُۥ لَلْحُسْنَىٰ ۚ فَلَنُنَبِّئَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِمَا عَمِلُوا۟ وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ
Na pindi tukimwonjesha rehema itokayo kwetu baada ya dhara kumgusa, bila ya shaka husema: 'Haya nayastahiki mimi, wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja. Na hata nikirudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nina mema yangu kwake!' Basi kwa yakini tutawaelezea wale waliokufuru hayo waliyoyatenda, na kwa yakini tutawaonjesha adhabu ngumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pindi tukimwonjesha rehema itokayo kwetu baada ya kumgusa dhara, bila ya shaka husema: Haya nayastahiki mimi, wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja. Na hata nikirudishwa kwa Mola wangu Mlezi bila ya shaka nina mema yangu kwake! Basi kwa yakini tutawaelezea walio kufuru hayo waliyo yatenda, na kwa yakini tutawaonjesha adhabu ngumu. [50]
[50] Tunaapa: Tukimwonjesha mtu neema, kwa fadhila yetu, baada ya dhara kubwa iliyo msibu bila ya shaka husema: Hii neema niliyo ipata ni haki yangu mimi. Wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja. Na ninaapa ikitokea nikarejeshwa kwa Mola wangu Mlezi basi na huko kwake bila ya shaka nitapata malipo mema. Lakini Sisi tunaapa: Hapana shaka tutawalipa walio kufuru, Siku ya Kiyama, kwa vitendo vyao! Na hapana shaka tutawaonjesha adhabu kali iliyo rindikwa juu kwa juu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tunapomuonjesha binadamu neema kutoka kwetu baada ya shida na mitihani, hamshukuru Allah Mtukufu Aliyetukuka bali anaruka mpaka na kusema, «Haya niliyoyapata yamenijia kwa kuwa mimi ninastahiki kuyapata, na sidhani kuwa Kiyama ni chenye kuja.» Anasema hayo kwa njia ya kukanusha kufufuliwa «Na tukichukulia kuwa Kiyama kitakuja na kuwa mimi nitarudi kwa Mola wangu, basi nitapata Pepo Kwake.» Basi tutawapasha habari wale walioikanusha Siku ya Kiyama kwa yale maovu waliyoyafanya, na tutawaonjesha adhabu kali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net