Fussilat 41:49
فصلتلَّا يَسْـَٔمُ ٱلْإِنسَـٰنُ مِن دُعَآءِ ٱلْخَيْرِ وَإِن مَّسَّهُ ٱلشَّرُّ فَيَـُٔوسٌ قَنُوطٌ
Mwanadamu hachoki kuomba dua za heri, na inapompata shari, mara huvunjika moyo mno akakata tamaa sana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwanaadamu hachoki kuomba dua za kheri, na inapo mpata shari, mara huvunjika moyo akakata tamaa. [49]
[49] Mwanaadamu hachoki kumwomba Mola wake Mlezi kwa kheri za kidunia. Ikimpata shari basi huwa mwingi wa kuikatia tamaa kheri, na kuvunjika moyo hadi, ya kwamba Mwenyezi Mungu hamwitikii dua yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Binadamu hachoki kumuomba Mola wake Ampatie mema ya duniani, na akipatwa na umasikini na shida, huwa anakata tamaa na rehema za Allah Mtukufu na anakufa moyo kwa kuwa na dhana mbaya kwa Mola wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net