Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 30

Fussilat 41:30

فصلت

إِنَّ ٱلَّذِينَ قَالُوا۟ رَبُّنَا ٱللَّهُ ثُمَّ ٱسْتَقَـٰمُوا۟ تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا۟ وَلَا تَحْزَنُوا۟ وَأَبْشِرُوا۟ بِٱلْجَنَّةِ ٱلَّتِى كُنتُمْ تُوعَدُونَ

Maana

Hakika wale waliosema: "Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu!" Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Bustani mliyokuwa mkiahidiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyo kuwa mkiahidiwa. [30]

[30] Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, kwa kuukubali Upweke wake, kisha wakasimama sawa sawa juu ya sharia zake, Malaika watawateremkia mara kwa mara wakiwaambia: Msikhofu kukuteremkieni shari, wala msihuzunike kuwa mtakosa kheri, na furahini kuwa mtapata Pepo mliyo ahidiwa kwa ndimi za Manabii na Mitume.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika ya wale waliosema, Mola wetu ni Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Peke Yake kisha wakasimama imara kufuata Sheria Yake, Malaika watawateremkia wakati wa kufa waseme kuwaambia, «Msiogope kufa na yatakayokuwa baada yake, wala msiwe na masikitiko juu ya yale mtakayoyaacha nyuma yenu katika mambo ya kilimwengu, na furahikeni kwa pepo ambayo mlikuwa mkiahidiwa».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net