Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 28

Fussilat 41:28

فصلت

ذَٰلِكَ جَزَآءُ أَعْدَآءِ ٱللَّهِ ٱلنَّارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا دَارُ ٱلْخُلْدِ ۖ جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا يَجْحَدُونَ

Maana

Hayo ndiyo malipo ya Maadui wa Mwenyezi Mungu - Moto! Humo watakuwa na maskani ya kudumu, ndiyo malipo yao kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara zetu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ndiyo malipo ya Maadui wa Mwenyezi Mungu - Moto! Humo watakuwa na maskani ya kudumu, ndiyo malipo yao kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara zetu. [28]

[28] Hizo adhabu zilizo tajwa ni malipo wanayo stahiki maadui wa Mwenyezi Mungu - Moto walio andaliwa katika makaazi ya kuishi milele, kuwa ni malipo kwa kule kuzikataa mfululizo Ishara za Mwenyezi Mungu na hoja zake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Malipo haya ambayo watalipwa waliokufuru ni malipo ya maadui wa Allah Mtukufu, nayo ni Moto utakaokuwa nyumba yao ya kukaa daima milele, ukiwa ni malipo ya wale waliokuwa wakizikanusha hoja zetu na dalili zetu. Na aya hii inatolea ushahidi ukubwa wa kosa la mwenye kuwapotosha watu na Qur’ani tukufu na kuwazuia wasiizingatie wala wasijiongoze nayo kwa njia yoyote iwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net