Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 27

Fussilat 41:27

فصلت

فَلَنُذِيقَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ عَذَابًا شَدِيدًا وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَسْوَأَ ٱلَّذِى كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Basi hapana shaka tutawaonjesha hao waliokufuru adhabu kali, na hapana shaka tutawalipa malipo mabaya zaidi kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi hapana shaka tutawaonjesha hao walio kufuru adhabu kali, na hapana shaka tutawalipa malipo mabaya ya yale waliyo kuwa wakiyafanya. [27]

[27] Tunaapa: Bila ya shaka tutawaonjesha walio kufuru adhabu kali kwa vitendo vyao, na khasa kwa hivi kuipiga vita Qur'ani. Na bila ya shaka tutawalipa malipo maovu kabisa kwa vitendo vyao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi Tutawaonjesha, tena tutawaonjesha, wale waliosema neno hili adhabu kali, duniani na Akhera, na tutawalipa, tena tutawalipa, mabaya zaidi ya makosa waliokuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net