An-Nisaa 4:76
النساءٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ يُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱلطَّـٰغُوتِ فَقَـٰتِلُوٓا۟ أَوْلِيَآءَ ٱلشَّيْطَـٰنِ ۖ إِنَّ كَيْدَ ٱلشَّيْطَـٰنِ كَانَ ضَعِيفًا
Wale walioamini wanapigana vita katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wale waliokufuru wanapigana vita katika njia ya Twaghut. Basi piganeni na marafiki wa Shetani. Hakika, hila ya Shetani ni dhaifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapiana katika njia ya upotofu. Basi piganeni na marafiki wa Shet'ani. Hakika hila za Shet'ani ni dhaifu. [76]
[76] Walio isadiki Haki na wakaifuata, hupigana kwa ajili ya kulitukuza Neno la Mwenyezi Mungu, na uadilifu, na Haki. Na wale wanao pinga wakafanya inadi hupigana kwa ajili ya dhulma na uharibifu. Kwa hivyo hawa wamekuwa ni vipenzi vya Shetani. Basi enyi Waumini! Wapigeni vita hao, kwani wao ni wenzake Shetani na wasaidizi wake. Na jueni kuwa nyinyi mtawashinda tu kwa kuungwa mkono na Mwenyezi Mungu, kwani mpango wa Shetani, na ingawa mkubwa vipi ufisadi wake, ni dhaifu, hauna nguvu. Na Haki ndiyo yenye ushindi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale walio wakweli katika Imani zao, kiitikadi na kivitendo, wanapigana jihadi katika njia ya kuitetea haki na watu wake, na wale waliokufuru wanapigana katika njia ya uonevu na uharibifu katika ardhi. Basi wapigeni vita watu wa ukafiri na ushirikina wanaomfuata Shetani na kutii amri yake. Hakika mipango ya Shetani anayowapangia wafuasi wake ni dhaifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net