An-Nisaa 4:70
النساءذَٰلِكَ ٱلْفَضْلُ مِنَ ٱللَّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ عَلِيمًا
Hiyo ndiyo fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kwamba ndiye Mwenye kujua vyema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hiyo ni fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kutosha. [70]
[70] Hayo ni makao matukufu kwa mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hiyo ni fadhila kubwa inayo tokana na Mwenyezi Mungu. Naye anavijua sana vitendo vyenu, naye atakulipeni kwavyo. Yamtosha Muumini kuwa Mwenyezi Mungu anamjua, naye lake ni kumt'ii Mola wake Mlezi na kutafuta radhi zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Vipewa vingi hivyo vinatoka kwa Allah Mtukufu Peke Yake. Na inatosha kuwa Allah Mtukufu ni Mjuzi, Anazijua hali za waja Wake na Anawajua wenye kustahiki thawabu nyingi kati yao kwa matendo mema waliyoyafanya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net