An-Nisaa 4:69
النساءوَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّـٰلِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُو۟لَـٰٓئِكَ رَفِيقًا
Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, basi hao wako pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi (Wakweli), na Mashahidi (watu waliouawa kwa ajili ya dini), na Watu wema. Na hao ndio wenza wazuri mno!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao! [69]
[69] Na mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume kwa kuzifuata kwa unyenyekevu amri zao na kuridhia hukumu yao, basi huyo yu pamoja na alio waneemesha Mwenyezi Mungu kwa uwongofu na kuwawezesha duniani na Akhera. Na watu hao ni Manabii wake, na wafuasi wao walio wasadiki na kuwakubali na wakafuata nyendo zao, na Mashahidi walio kufa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na watu wema watendao mema kwa siri na dhaahiri. Na hapana la kushinda uzuri kuliko kuwa pamoja na watu hawa - haingii mashakani mwenye kukaa nao, wala hayachoshi mazungumzo yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mwenye kukubali amri za Allah Mtukufu na uongofu wa Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, basi hao ni wale ambao wana utukufu wa mambo na vyeo. Wao watakuwa pamoja na wale waliopewa neema na Allah Mtukufu miongoni mwa Mitume na wakweli wa Imani, ambao kuamini kwao yaliyoletwa na Mitume kulikamilika kiitikadi, kimaneno na kivitendo na mashahidi katika njia ya Allah Mtukufu na Waumini wema. Na wazuri wa marafiki wa mtu kuwa nao Peponi ni hao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net