An-Nisaa 4:5
النساءوَلَا تُؤْتُوا۟ ٱلسُّفَهَآءَ أَمْوَٰلَكُمُ ٱلَّتِى جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمْ قِيَـٰمًا وَٱرْزُقُوهُمْ فِيهَا وَٱكْسُوهُمْ وَقُولُوا۟ لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا
Wala msiwape wasio na akili mali zenu ambazo Mwenyezi Mungu amezifanya kuwa za kuwakimu. Na walisheni kutoka kwazo, na wavisheni, na waambieni kauli njema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu. Walisheni katika hayo na muwavike, na mseme nao maneno mazuri. [5]
[5] Wala msiwape wasio na akili ya kutosha kuendesha mambo yao mali yao, nayo ni mali yenu vile vile. Kwani mali ya yatima na ya mchache wa akili yamekulazimuni myatazame yasiharibike. Mwenyezi Mungu ameyajaalia mali hayo ya kukimu maisha. Wapeni kutokana na pato lake sehemu kama wanavyo hitajia kwa kula, na wavisheni na muwatendee vyema, na mseme nao maneno ya kuwaridhisha sio ya kuwaudhi au kuwadhili.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala msiwape, enyi wasimamizi, wale wafujaji, kati ya wanaume, wanawake na watoto, mali zao ambazo ziko chini ya mikono yenu, kwani wataziweka sehemu isiyokuwa yake. Mali hizi ndizo ambazo juu yake yanasimama maisha ya watu. Wapeni matumizi na mavazi, kwenye mali hizo, na muwaambie maneno mazuri yanayopendeza na muamiliane nao kwa tabia njema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net