An-Nisaa 4:170
النساءيَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدْ جَآءَكُمُ ٱلرَّسُولُ بِٱلْحَقِّ مِن رَّبِّكُمْ فَـَٔامِنُوا۟ خَيْرًا لَّكُمْ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا۟ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا
Enyi Watu! Hakika, amekwishawajia Mtume huyu kwa haki kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, ndiyo heri kwenu. Na mkikufuru, basi hakika ni vya Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na ardhi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi Watu! Amekwisha kujieni Mtume huyu na haki itokayo kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, ndiyo kheri yenu. Na mkikakanusha basi hakika viliomo mbinguni na duniani ni vya Mwenyezi Mungu tu. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. [170]
[170] Enyi watu! Amekwisha kukujieni Mtume huyu, Muhammad, na Dini ya Haki kutokana na Mola Mlezi wenu. Basi yaaminini aliyo kuja nayo; ndiyo itakuwa kheri yenu. Na pindi mkikataa ila kukufuru tu, basi mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkwasi na imani yenu, hana haja nayo. Yeye ndiye Mwenye kukumilikini nyinyi. Kwani vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi ni vyake Yeye, kwa kuvimiliki, kuviumba na kuviendesha atakavyo. Naye ni Mwenye kuvijua vyema viumbe vyake, ni Mwenye hikima katika uendeshaji wake. Haupotezi ujira wa mwema, wala hapuuzi kumlipa mwovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi watu, amewajia nyinyi Mjumbe wetu,Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na Uislamu, Dini ya haki, kutoka kwa Mola wenu, basi ikubalini na muifuate, kwani kuiyamini ni bora kwenu. Na iwapo mtaendelea na ukafiri wenu, basi Allah Mtukufu ni Mkwasi, Hana haja nanyi, na pia Hana haja ya kuamini kwenu, kwa kuwa Yeye ni Mmiliki wa vilivyo mbinguni na ardhini. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi mno wa maneno yenu na vitendo vyenu, ni Mwingi wa hekima katika uwekaji Sheria Wake na amri Zake. Na iwapo mbingu na ardhi zimemnyenyekea Allah Mtukufu, Aliyetukuka, katika kuwa na kukadiriwa, kama viumbe vyingine vyote vilivyomnyenyekea, basi ni bora kwenu mumwamini Allah Mtukufu na Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, muiamini Qur’ani Aliomteremshia na muifuate Dini hiyo kisheria hadi ulimwengu wote uwe ni wenye kumnyenyekea Allah Mtukufu kwa mpango uliokadiriwa na kisheria. Katika aya hii kuna dalili ya kuwa ujumbe wa Nabii wa Allah Mtukufu na Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, unakusanya ulimwengu wote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net