Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 9

Az-Zumar 39:9

الزمر

أَمَّنْ هُوَ قَـٰنِتٌ ءَانَآءَ ٱلَّيْلِ سَاجِدًا وَقَآئِمًا يَحْذَرُ ٱلْـَٔاخِرَةَ وَيَرْجُوا۟ رَحْمَةَ رَبِّهِۦ ۗ قُلْ هَلْ يَسْتَوِى ٱلَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَٱلَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَـٰبِ

Maana

Je, afanyaye ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi... Sema: Ati watakuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Hakika wanaokumbuka ni watu wenye akili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake MleziSema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili. [9]

[9] Je! Mwenye kumnyenyekea Mwenyezi Mungu nyakati za usiku anao upitisha na hali yeye yumo kusujudu na kusimama, akiiogopa Akhera, naye anataraji rehema ya Mola wake Mlezi, ni kama anaye mwomba Mola wake Mlezi wakati wa shida na akamsahau wakati wa neema? Ewe Muhammad! Waambie: Ati wanakuwa sawa wenye kujua haki za Mwenyezi Mungu wakamuabudu Yeye tu peke yake, na wale wasio jua wakapuuza kuziangalia Ishara? Hakika wenye akili nzuri ndio wanao waidhika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, kafiri huyu anayejistarehesha na ukafiri wake ndiye bora au ni yule anayemuabudu Mola wake na kumnyenyekea, anatumia nyakati za usiku kusimama kwenye Ibada na kumsujudia, anaogopa adhabu ya Akhera na kutarajia rehema ya Mola wake? Sema, ewe Nabii, «Je, wanalingana wale wanaomjua Mola wao na dini yao ya haki na wale wasiojua chochote katika hayo?» Hawalingani. Kwa hakika wanaokumbuka na kujua tafauti ni wale wenye akili timamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net