Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 8

Az-Zumar 39:8

الزمر

وَإِذَا مَسَّ ٱلْإِنسَـٰنَ ضُرٌّ دَعَا رَبَّهُۥ مُنِيبًا إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا خَوَّلَهُۥ نِعْمَةً مِّنْهُ نَسِىَ مَا كَانَ يَدْعُوٓا۟ إِلَيْهِ مِن قَبْلُ وَجَعَلَ لِلَّهِ أَندَادًا لِّيُضِلَّ عَن سَبِيلِهِۦ ۚ قُلْ تَمَتَّعْ بِكُفْرِكَ قَلِيلًا ۖ إِنَّكَ مِنْ أَصْحَـٰبِ ٱلنَّارِ

Maana

Na taabu inapomfikia mtu humwomba Mola wake Mlezi naye ameelekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake, husahau yale aliyokuwa akimwomba zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watu mbali na njia yake. Sema: Starehe na ukafiri wako kwa muda mchache. Kwani hakika wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na taabu inapo mfikia mtu humwomba Mola wake Mlezi naye ameelekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake, husahau yale aliyo kuwa akimwitia zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watu njia yake. Sema: Starehe na ukafiri wako kwa muda mchache. Kwani hakika wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni. [8]

[8] Na mtu akifikiwa na shida yoyote katika shida za dunia humwomba Mola wake Mlezi, na hurejea kwake, baada ya kuwa akimpuuza. Kisha Mola wake Mlezi akimpa neema kubwa husahau zile taabu alizo kuwa akimwombea Mola wake Mlezi amwondolee na amfarijie kabla hajamneemesha kwa neema hizo. Na humfanyia Mwenyezi Mungu miungu washirika walio sawa na Yeye kwa kuwaabudu. Huyo mtu hufanya haya ili ajipoteze yeye na wenginewe waiache Njia ya Mwenyezi Mungu. Ewe Muhammad! Mwambie huyo mwenye sifa hizi kwa kumwonya: Starehe na huko kuzikanya kwako neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yako kwa muda mchache. Kwani hakika wewe ni katika watu wa Motoni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na binadamu akipatwa na balaa, shida na maradhi humkumbuka Mola wake akataka nusura Yake na akamuomba, kisha Akimjibu na Akamuondolea shida yake na akampa neema Zake, huwa yuwasahau yale maombi yake aliyoyafanya kwa Mola wake alipomhitajia, na akawa anamshirikisha mwingine pamoja na Yeye, ili ampoteze mwingine amuepushe na kumuamini Allah Mtukufu na kumtii. Mwambie, ewe Mtume, kwa kumuonya, «Starehe na ukafiri wako muda mchache mpaka kufa kwako na kumalizika kipindi chako cha kuishi, hakika wewe ni miongoni mwa watu wa Motoni wenye kukaa milele humo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net