Az-Zumar 39:64
الزمرقُلْ أَفَغَيْرَ ٱللَّهِ تَأْمُرُوٓنِّىٓ أَعْبُدُ أَيُّهَا ٱلْجَـٰهِلُونَ
Sema: Je, mnaniamrisha nimuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, enyi majahili?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Je! Mnaniamrisha nimuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu, enyi majaahili? [64]
[64] Ewe Muhammad! Sema: Je! Baada ya kuweka wazi Ishara zote kuwepo Mwenyezi Mungu Mmoja wa kuabudiwa, mnaniamrisha nimuabudu mwenginewe, enyi wajinga, majaahili?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, uwaambie washirikina wa watu wako, «hivi yule asiyekuwa Allah Mtukufu, enyi wajinga, mnanishauri nimuabudu na hali ibada haifai kufanyiwa kitu chochote isipokuwa Yeye?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net