Az-Zumar 39:63
الزمرلَّهُۥ مَقَالِيدُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ
Yeye anazo funguo za mbingu na ardhi. Na wale waliozikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye kuhasiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye anazo funguo za mbingu na ardhi. Na wale walio zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye kukhasiri. [63]
[63] Maendesho ya mambo ya katika mbingu na ardhi yako kwa Mwenyezi Mungu. Hayaendeshi hayo isipo kuwa Yeye. Na makafiri kwa hoja za Mwenyezi Mungu na ushahidi wake ndio wao, peke yao, ndio wenye kukhasiri, mwisho wa kukhasiri! (Injili ya Mathayo 16:16-20 imedai kuwa Yesu kampa funguo za mbingu na ardhi Petro, na hivyo ndiyo Papa wa Roma amerithi funguo hizo na kuanzisha Kanisa la Kikatoliki, na uwezo wa kufutia watu dhambi na kuwaangamiza Motoni. Marcello Craveri, mtaalamu wa Biblia wa Kitaliana ameandika katika kitabu chake Maisha ya Yesu (sahifa 227-28 Panther Edn.) kuwa Mathayo 16:16-20 imeongezwa na ametoa hoja 7 kwa wazo hilo. Licha ya kuwa Yesu hakumpa Petro hizo funguo za mbingu na ardhi, yeye mwenyewe Yesu hakuwa nazo.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni za Allah Mtukufu funguo za hazina za mbinguni na ardhini, Anatoa kutoka kwenye hazina hizo kuwapa viumbe Vyake namna Anavyotaka. Na wale waliozikanusha aya za Qur’ani na dalili za wazi zilizomo, hao ndio wenye kupata hasara ulimwenguni kwa kutoafikiwa kuamini, na kesho Akhera kwa kukaa milele Motoni.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net