Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 52

Az-Zumar 39:52

الزمر

أَوَلَمْ يَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Maana

Kwani wao hawajui kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na kumkunjia? Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaoamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwani wao hawajui kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na akamkadiria? Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao amini. [52]

[52] Je! Hawa wanasema wayasemayo, wala hawajui kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humpa kwa kadiri atakacho kwa mujibu wa hikima yake? Hakika katika haya bila ya shaka ni mazingatio kwa watu wanao amini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hao hawajui kwamba riziki ya Allah Mtukufu kwa binadamu haimaanishi kuwa aliyeruzukiwa ana hali njema, na kwamba Allah Mtukufu Ana hekima nyingi? na kwamba anamkunjulia riziki Anayemtaka katika waja Wake, awe mwema au muovu, na anampunguzia Anayemtaka katika wao? Hakika katika kukunjua na kupunguza riziki kuna dalili zilizo wazi kwa watu wanaoamini amri ya Allah Mtukufu na kuifanyia kazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net