Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 51

Az-Zumar 39:51

الزمر

فَأَصَابَهُمْ سَيِّـَٔاتُ مَا كَسَبُوا۟ ۚ وَٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مِنْ هَـٰٓؤُلَآءِ سَيُصِيبُهُمْ سَيِّـَٔاتُ مَا كَسَبُوا۟ وَمَا هُم بِمُعْجِزِينَ

Maana

Basi ukawasibu uovu wa yale waliyoyachuma. Na wale waliodhulumu miongoni mwa hawa utawasibu uovu wa yale waliyoyachuma vile vile. Nao si wenye kushinda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi ukawasibu uovu wa waliyo yachuma. Na wale walio dhulumu miongoni mwa hawa utawasibu uovu wa waliyo yachuma vile vile. Nao si wenye kushinda. [51]

[51] Yakawasibu makafiri walio tangulia malipo ya madhambi ya vitendo vyao, na madhaalimu miongoni mwa hawa wanao semezwa hivi sasa yatawapata vile vile malipo ya madhambi ya vitendo vyao. Wala hawa hawataiepuka adhabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yakawapata wale waliyosema kauli hii, miongoni mwa ummah waliopita, mateso ya matendo mabaya waliyoyachuma, hivyo basi wakaharakishiwa laana katika maisha ya duniani. Na wale waliojidhulumu nafsi zao katika watu wako, ewe Mtume, na wakasema kauli hii, yatawapata mateso ya yale mabaya waliyoyachuma kama yaliyowapata waliokuwa kabla yao, na hawakuwa wao ni wenye kumponyoka Allah Mtukufu wala kumshinda.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net