Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 41

Az-Zumar 39:41

الزمر

إِنَّآ أَنزَلْنَا عَلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ لِلنَّاسِ بِٱلْحَقِّ ۖ فَمَنِ ٱهْتَدَىٰ فَلِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ

Maana

Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa Haki. Kwa hivyo, mwenye kuongoka, ni kwa faida ya nafsi yake. Na mwenye kupotoka, bila ya shaka amepotoka kwa hasara yake. Na wewe si mlinzi juu yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa Haki. Basi mwenye kuongoka ni kwa nafsi yake, na mwenye kupotoka bila ya shaka amepotoka kwa khasara yake. Na wewe si mlinzi juu yao. [41]

[41] Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani Tukufu hii kwa watu wote, nayo imekusanya Haki iliyo thibiti. Basi mwenye kuongoka kwa sababu yake basi manufaa hayo ni kwa nafsi yake, na mwenye kuipotea njia yake basi balaa ya upotofu wake itamrejea mwenyewe. Wala wewe, Muhammad, si mwenye kuwakilishwa uwongofu wao. Jukumu lako ni kufikisha ujumbe, nao umeufikisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika sisi tumekuteremshia wewe, ewe Mtume, Qur’ani kwa haki ikiwa ni yenye kuwaongoza viumbe wote kwenye njia ya uongofu. Basi mwenye kuongoka kwa mwangaza wake na akayatumia yaliyomo ndani yake na akasimama imara kufuata njia yake, basi manufaa ya kufanya hilo yatamrudia mwenyewe. Na mwenye kupotea baada ya kubainikiwa na uongofu, basi madhara yake yatamrudia mwenyewe, na hilo halitamdhuru Allah Mtukufu kitu chochote. Na hukuwa wewe, ewe Mtume, ni mwakilishwa wa kuyatunza matendo yao, kuwahesabu kwa hayo na kuwalazimisha unayoyataka, jukumu lako wewe si lingine isipokuwa ni kufikisha ujumbe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net