Az-Zumar 39:40
الزمرمَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُّقِيمٌ
Ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi na itakayemshukia adhabu ya daima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ni nani itakaye mfikia adhabu ya kumhizi, na itakaye mshukia adhabu ya daima. [40]
[40] Waambie, kwa kuwapa ahadi: Enyi watu! Ishikilieni hiyo hiyo njia yenu ya ukafiri na kukadhibisha, na mimi hakika ninashikilia aliyo niamrisha Mola wangu Mlezi. Mtakuja ona nani katika sisi atakaye fikiwa na adhabu ya kumdhalilisha, na atakaye teremkiwa na adhabu ya daima isiyo mwondokea?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mtajua ni yupi atakayejiwa na adhabu yenye kumfanya mnyonge katika maisha ya ulimwenguni, na atakayeshukiwa na adhabu ya daima kesho Akhera, haitamuepuka wala haitamuondokea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net