Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 36

Az-Zumar 39:36

الزمر

أَلَيْسَ ٱللَّهُ بِكَافٍ عَبْدَهُۥ ۖ وَيُخَوِّفُونَكَ بِٱلَّذِينَ مِن دُونِهِۦ ۚ وَمَن يُضْلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنْ هَادٍ

Maana

Je, Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake? Na ati wanakutishia kwa hao wenginewe wasiokuwa Yeye! Na aliyepotezwa na Mwenyezi Mungu, basi hana wa kumwongoa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake? Na ati wanakutishia kwa hao wenginewe wasio kuwa Yeye! Na aliye hukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea hana wa kumwongoa. [36]

[36] Mwenyezi Mungu, peke yake, ni Mwenye kuwatosheleza waja wake kwa kila lilio wakhusu. Na ati hao makafiri wa Kikureshi wanakutisha, ewe Muhammad, kwa miungu yao wanayo iomba badala ya Mwenyezi Mungu. Na hayo ni katika upotovu wao. Na mwenye kupotozwa na Mwenyezi Mungu, kwa kumjua kuwa huyo amekhiari upotovu kuliko uwongofu, basi hatakuwa na mwongozi wa kumwongoza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hivi Allah Mtukufu si Mwenye kumtosheleza mja Wake Muhammad vile vitisho vya washirikina na vitimbi vyao kuwa wao hawatamfikia kwa ubaya wowote? Ndio, Yeye Atamtosheleza katika jambo la Dini yake na dunia yake, na Atamtetea dhidi ya yoyote anayemtaka kwa ubaya. Na wao wanakutisha, ewe Mtume, na waungu wao wanaodai kuwa watakudhuru. Na yoyote yule ambaye Allah Mtukufu Ameondoa msaada Wake kwake na Akamfanya apotee njia ya haki, basi huyo hana muongozi wa kumuongoza Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net