Az-Zumar 39:35
الزمرلِيُكَفِّرَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ أَسْوَأَ ٱلَّذِى عَمِلُوا۟ وَيَجْزِيَهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ ٱلَّذِى كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Ili Mwenyezi Mungu awafutie ukomo wa uovu walioufanya na awalipe ujira wao kwa mujibu wa ukomo wa wema waliokuwa wakiutenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ili Mwenyezi Mungu awafutie ukomo wa uovu walio ufanya na awalipe ujira wao kwa mujibu wa ukomo wa wema walio kuwa wakiutenda. [35]
[35] Mwenyezi Mungu amewakirimu wachamngu kwa alivyo wakirimu, ili awafutie vile vitendo vyao viovu kabisa, na awalipe ujira wao kwa bora ya vitendo vyao walivyo vitenda duniani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ili Allah Mtukufu Awafutie yale maovu zaidi ya matendo waliyoyafanya ulimwenguni, kwa sababu ya kile walichokifanya cha kurudi kwa Allah Mtukufu, kwa kutubia makosa waliyoyatenda huko, na ili Allah Mtukufu Awalipe mema, kwa utiifu wao ulimwenguni, malipo mazuri zaidi ya matendo ambayo walikuwa wakiyafanya, nayo ni Pepo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net