Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 21

Az-Zumar 39:21

الزمر

أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَسَلَكَهُۥ يَنَـٰبِيعَ فِى ٱلْأَرْضِ ثُمَّ يُخْرِجُ بِهِۦ زَرْعًا مُّخْتَلِفًا أَلْوَٰنُهُۥ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَىٰهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَجْعَلُهُۥ حُطَـٰمًا ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ

Maana

Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni. Kisha akayapitisha kwenye chemchemi katika ardhi, kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbalimbali? Kisha hunyauka ukaiona imekuwa kimanjano, na kisha huifanya mapepe. Bila ya shaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye akili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni. Kisha akayapitisha kwenye chemchem katika ardhi, kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbali mbali? Kisha hunyauka ukaiona imekuwa kimanjano, na kisha huifanya mapepe. Bila ya shaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye akili. [21]

[21] Ewe usemezwaye! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni, akayapitisha kwenye mito na chemchem za katika ardhi, kisha kwa maji hayo akaotesha mimea ya namna mbali mbali. Kisha baada ya kustawi kwake hiyo mimea, ikayabisika ukaiona imekuwa rangi ya manjano baada ya kustawi kwake. Kisha akaifanya imevurugika na kukatika vipande vipande. Hakika kutoka kwenye hali moja na kuingia hali nyengine ni mazingatio kwa wenye akili zilizo nawirika. Huku kuzunguka maji katika maumbile kutoka mbinguni na kufika kwenye ardhi na huko yakenda chini na kutimbuka katika chemchem, hakukuwa kunajuulikana kabla ya katikati za karne ya nane tangu kuzaliwa Nabii Isa a.s. Fikra iliyo zagaa kabla ya hapo ni kuwa maji ya chemchem na mito yanatimbuka kutoka chini ya ardhi kutoka kwenye mashimo na visima katika vina vya bahari.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, huoni, ewe Mtume, kuwa Allah Mtukufu Anateremsha mvua kutoka mawinguni, akaitia ardhini, akaifanya ni mikondo yenye kuchimbuka na maji yenye kutiririka, kisha anatoa kwa maji hayo mimea yenye rangi tafauti na aina mbalimbali, kisha inakauka baada ya ubichi wake na mng’aro wake, hapo utaiona imebadilika kuwa rangi ya manjano, kisha Anaifanya kuwa niyenye kuvunjikavunjika na kumumunyuka? Kwa hakika, katika kitendo hicho cha Allah Mtukufu pana ukumbusho na mawaidha kwa wenye akili timamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net