Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 20

Az-Zumar 39:20

الزمر

لَـٰكِنِ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ رَبَّهُمْ لَهُمْ غُرَفٌ مِّن فَوْقِهَا غُرَفٌ مَّبْنِيَّةٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۖ وَعْدَ ٱللَّهِ ۖ لَا يُخْلِفُ ٱللَّهُ ٱلْمِيعَادَ

Maana

Lakini waliomcha Mola wao Mlezi watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa; chini yake hupita mito. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini walio mcha Mola wao Mlezi watapata ghorofa zilizo jengwa juu ya ghorofa; chini yake hupita mito. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. [20]

[20] Lakini wenye kumkhofu Mola wao Mlezi watapata vyeo vya juu Peponi na majumba yake ya fakhari, yenye kupitiwa chini yake na mito. Hiyo ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu haendi kinyume na ahadi yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lakini wale waliomcha Mola wao, kwa kumtii na kwa kumtakasia ibada, watakuwa na vyumba, huko Peponi, vilivyojengewa baadhi yake juu ya vingine, ambavyo chini ya miti yake mito inapita. Allah Mtukufu amewaahidi (vyumba hivyo) waja Wake wachamungu, ahadi ambayo ni yenye kutimia kwa uhakika, na Allah Mtukufu Haendi kinyume na ahadi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net