As-Saaffaat 37:6
الصافاتإِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنْيَا بِزِينَةٍ ٱلْكَوَاكِبِ
Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. [6]
[6] Sisi tumeipamba hii mbingu ya karibu na watu wa duniani kwa mapambo, nayo ni hizo nyota zinazong'ara, zenye ukubwa mbali mbali, na mwahala pao mbali mbali kwenye anga la ulimwengu kama ionekanavyo kwa macho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net