As-Saaffaat
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنْيَا بِزِينَةٍ ٱلْكَوَاكِبِ 6 وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَـٰنٍ مَّارِدٍ 7 لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلْمَلَإِ ٱلْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ 8 دُحُورًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ 9
{6 - 9} "Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. Na kulinda na kila shetani muasi. Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu." Mwenyezi Mungu alizitaja faida kuu mbili hizi kuhusu nyota: Moja yake ni kwamba ni pambo la mbingu. Kwani lau kuwa si hizo, mbingu ingelikuwa na giza bila ya mwangaza wowote. Lakini alizifanya kuwa pambo la mbingu ili pande zake zipate kuangazwa na ziwe na sura nzuri. Pia watu huongozwa kwazo katika viza vya nchi kavu na baharini, na pia kuna manufaa mbalimbali yanayopatikana humo. Ya pili ni kuzilinda mbingu kutokana na kila shetani muasi ambaye uasi wake unafikia kwenda kusikia maneno ya viumbe watukufu wa juu kabisa, ambao ni Malaika. Lakini wakitaka kusikiliza, wanaupiwa vimondo vinavyong'ara "kutokea kila upande" ili kuwafukuza na kuwaweka mbali na suala la kusikiliza kile kinachosemwa na viumbe watukufu wa juu kabisa. "Na wanayo adhabu ya kudumu." kwa sababu waliasi kumtii Mola wao Mlezi.