Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 37 · Aya ya 29

As-Saaffaat 37:29

الصافات

قَالُوا۟ بَل لَّمْ تَكُونُوا۟ مُؤْمِنِينَ

Maana

Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini. [29]

[29] Watasema walio jipa ukubwa: Sisi hatukukugeuzeni njia, lakini nyinyi wenyewe mliikataa Imani, na mkaipuuza kwa khiari yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo watasema wafuatwa kuwaambia wafuasi, «Mambo si kama vile mnavyodai, bali ni nyoyo zenu zilikuwa zimekataa kuamini, zimeuelekea ukafiri na uasi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Saaffaat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net