Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 37 · Aya ya 28

As-Saaffaat 37:28

الصافات

قَالُوٓا۟ إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ ٱلْيَمِينِ

Maana

Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia. [28]

[28] Wanyonge watawaambia walio jipa ukubwa: Nyinyi mlikuwa mkitujia upande tulio udhania ni wa kheri na mafanikio, ili mtugeuze njia tuache Haki twende kwenye upotovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wafuasi watasema kuwaambia wafuatwa, «Nyinyi mlikuwa mkitujia kwa upande wa dini na haki, mkiiponda sheria kwetu, mkitutia chuki nayo na mkitupambia upotevu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Saaffaat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net