As-Saaffaat 37:145
الصافاتفَنَبَذْنَـٰهُ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمٌ
Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa. [145]
[145] Tukamtupa pahali patupu kwenye nchi pasipo kuwa na miti wala majumba, naye ni mgonjwa kwa yaliyo mpata. Yaliyo mtokea Sayyidna Yunus a.s. ni muujiza. Lakini nayo si muhali kutokea mtu kumezwa na samaki, na akabakia yuhai ndani yake kwa muda fulani. Mawili yaweza kuwa - Kwanza, ni kuwa huyo samaki ni namna asiye kuwa na meno katika kabila ya nyangumi wakubwa kabisa, kama nyangumi wanao onekana sana katika Bahari ya Kati (Mediterranean). Urefu wake huweza kufika Mita 20. Alibaki Yunus katika mpandikizi wa kinywa chake huyo nyangumi mpaka alipo mtema kwenye ufukwe mtupu, kwani koo ya nyangumi ni nyembamba hawezi kupita mtu. Pili, yaweza kuwa huyo samaki ni namna ya wenye meno pia, kama nyangumi wa ambari, na ambaye pia urefu wake hufika mita 20. Hawa mara kadhaa wa kadhaa huonekana katika Bahari ya Kati. Nyangumi hao yawezekana kwa kawaida kuwameza wanyama wakubwa wanao pita urefu wa mita tatu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tukamtoa kwenye tumbo la chewa na tukamtupa kwenye ardhi tupu, isiyokuwa na miti wala majengo, akiwa dhaifu wa mwili.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net