As-Saaffaat 37:144
الصافاتلَلَبِثَ فِى بَطْنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
Bila ya shaka angelikaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa. [144]
[144] Na lau kuwa Yunus hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu, wanao dumu kumdhukuru, angeli kufa ndani ya samaki, wala asingeli toka humo mpaka siku ya kufufuliwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Angekaa ndani ya tumbo la chewa, na lingekua ni kaburi lake mpaka Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net