Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 37 · Aya ya 11

As-Saaffaat 37:11

الصافات

فَٱسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَآ ۚ إِنَّا خَلَقْنَـٰهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍۭ

Maana

Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tuliowaumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unaonata.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata. [11]

[11] Ewe Nabii! Hebu waulize hao wanao kanya kufufuliwa wanao ona hayawi hayo: Je! Kwani kuwaumba wao hawa ni kugumu zaidi au kuziumba mbingu, na ardhi, na nyota, na vyenginevyo, tulivyo viumba Sisi?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi waulize, ewe Mtume, wenye kukanusha Kufufuliwa: Je kuumbwa kwao ni kugumu zaidi au ni hivi viumbe tulivyoviumba? Kwa hakika, tulimuumba baba yao Ãdam kwa udongo ulioshikana na kuambatana.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Saaffaat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net