As-Saaffaat 37:103
الصافاتفَلَمَّآ أَسْلَمَا وَتَلَّهُۥ لِلْجَبِينِ
Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji. [103]
[103] Yule baba na mwanawe walipo iridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu, na akamweka juu ya fungu la mchanga na akamlaza juu yake, kipaji chake kikawa juu ya ardhi, akawa tayari kumchinja.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walipojisalimisha wao wawili kwa kuifuata amri ya Allah Mtukufu, na Ibrãhîm Akamlaza Ismã’îl chini, kwa upande wa paji la uso, ili kumchinja.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net