Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 37 · Aya ya 102

As-Saaffaat 37:102

الصافات

فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعْىَ قَالَ يَـٰبُنَىَّ إِنِّىٓ أَرَىٰ فِى ٱلْمَنَامِ أَنِّىٓ أَذْبَحُكَ فَٱنظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَـٰٓأَبَتِ ٱفْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Maana

Basi alipofika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa, utanikuta mimi, Insha Allah (Mwenyezi Mungu akipenda), katika wanaosubiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri. [102]

[102] Akazaliwa huyo mwana, na alipo kuwa kijana wa kwenda naye baba yake katika kutafuta haja za maisha, Ibrahim alipewa mtihani kwa ndoto aliyo iota. Ibrahim akasema: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini ufunuo kutokana na Mwenyezi Mungu ananitaka nikuchinje! Basi wewe tazama unaonaje? Yule mwana mwema alisema: Ewe baba yangu! Tekeleza amri ya Mola wako Mlezi. Utaniona mimi katika wanao subiri, Inshallah!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Alipokuwa mkubwa Ismã‘îl, akawa anatembea na baba yake, baba yake alimwambia, «Mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja, je, una maoni gani?» (na ndoto za Manabii ni za kweli). Ismã‘îl akasema, kwa kumridhisha Mola wake, kumtii mzazi wake na kumsaidia juu ya utiifu kwa Allah Mtukufu, «Endelea katika jambo Alilokuamrisha Allah Mtukufu la kunichinja mimi. Utanikuta, Allah Mtukufu Akitaka, ni mvumilivu, mtiifu na ni mwenye kutarajia malipo mema (kutoka kwa Allah Mtukufu)».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Saaffaat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net