Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 54

Yaseen 36:54

يس

فَٱلْيَوْمَ لَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْـًٔا وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Maana

Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda. [54]

[54] Basi katika hii siku ya leo haipungukiwi nafsi na chochote katika ujira wake kwa kazi iliyo tenda. Na wala hamtopata isipo kuwa jaza ya mliyo kuwa mkiyatenda, ikiwa ni kheri au shari.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Katika Siku hiyo hesabu itakamilishwa kwa uadilifu. Hakuna nafsi itakayodhulumiwa kitu chochote, kwa kupunguzwa mema yake au kuongezwa maovu yake. Na hamtalipwa isipokuwa kwa yale mliokuwa mkiyafanya ulimwenguni.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net