Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 53

Yaseen 36:53

يس

إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَإِذَا هُمْ جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ

Maana

Haitakuwa isipokuwa ukelele mmoja tu, mara wote watahudhurishwa mbele yetu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watahudhuruishwa mbele yetu. [53]

[53] Wito wao wa kuwatoa hautakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watakusanywa mbele yetu wahudhurishwe ili tuwahisabie.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakutakuwa kufufuliwa huku isipokuwa ni matokeo ya mpulizo mmoja katika baragumu, punde si punde viumbe wote watasimama, watakuwa wamesimama mbele yetu wapate kuhesabiwa na kulipwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net