Yaseen 36:35
يسلِيَأْكُلُوا۟ مِن ثَمَرِهِۦ وَمَا عَمِلَتْهُ أَيْدِيهِمْ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ
Ili wale katika matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ili wale matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru? [35]
[35] Na humo tukafanya vitalu na mabustani ya mitende na mizabibu, na tukapasua humo chemchem ya kumwagia maji kwenye miti yake, na ikatoa matunda, na wao wakala katika hayo. Na hayo si kazi ya mikono yao. Basi kwa nini hawatoi haki ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yao kwa kumuamini na kumshukuru?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yote hayo ili waja wapate kula matunda yake. Na hayo hayakuwa isipokuwa ni rehema za Allah Mtukufu kwao, na si kwa harakati zao za kutafuta na bidii zao, wala si kwa hila zao na nguvu. Basi si wamshukuru Allah Mtukufu Aliyewaneemesha neema hizi ambazo hazihesabiki wala hazidhibitiki?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net