Yaseen 36:14
يسإِذْ أَرْسَلْنَآ إِلَيْهِمُ ٱثْنَيْنِ فَكَذَّبُوهُمَا فَعَزَّزْنَا بِثَالِثٍ فَقَالُوٓا۟ إِنَّآ إِلَيْكُم مُّرْسَلُونَ
Tulipowatumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: "Hakika sisi tumetumwa kwenu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu. [14]
[14] Tuliwatuma wajumbe wawili, wakawakadhibisha. Tukawaongeza nguvu kwa kumpeleka mwengine wa tatu. Basi hawa watatu wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tulipowatumia wajumbe wawili wawalinganie kumuamini Allah Mtukufu na kuacha kumuabudu asiyekuwa Yeye. Watu wa kijiji wakawakanusha wajumbe wawili hao tukawatilia nguvu kwa mjumbe wa tatu. Basi hao wajumbe watatu walisema kuwaambia watu wa kijiji, «Hakika sisi kwenu nyinyi,enyi watu, tumetumwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net