Yaseen 36:13
يسوَٱضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا أَصْحَـٰبَ ٱلْقَرْيَةِ إِذْ جَآءَهَا ٱلْمُرْسَلُونَ
Na wapigie mfano wa wakazi wa mji walipojiwa na Mitume.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa. [13]
[13] Ewe Nabii! Watajie watu wako kisa cha mji mmoja Kwani hicho ni kama kisa chao. Waliwaendea Wajumbe walio tumwa ili wawahidi (awaongoze). Baadhi wa wafasiri wanasema mji huo ni Antiokia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wapigie, ewe Mtume, washirikna wa watu wako wenye kukataa ulinganizi wako, mfano wa wao kuuzingatia, nao ni hadithi ya watu wa kijiji walipoendewa na wajumbe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net