Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 14

Faatir 35:14

فاطر

إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا۟ دُعَآءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا۟ مَا ٱسْتَجَابُوا۟ لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ

Maana

Mkiwaomba hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawawajibu. Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu. Na hapana atakayekupa habari vilivyo kama Yeye Mwenye habari.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia hawakujibuni. Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu. Na hapana atakaye kupa khabari vilivyo kama Yeye Mwenye khabari. [14]

[14] Mkiwaomba hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawasikii maombi yenu. Na hata ingeli kuwa wanasikia wasingeli kujibuni kitu chochote kwa hayo myatakayo. Na Siku ya Kiyama watakuja kukataa huo ushirikina wenu kuwashirikisha na Mwenyezi Mungu. Wala hapana wa kukupeni khabari za hali za Akhera kuliko huyo Mwenye kuzijua vyema kwa ujuzi wa ndani kabisa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mnapowaomba, enyi watu, waabudiwa hawa badala ya Allah Mtukufu, hawasikii maombi yenu, na lau wangesikia, kwa kukisia, wasingewaitikia, Na Siku ya Kiyama, watajiepusha na nyinyi. Na hakuna yoyote wa kukupasha habari, ewe Mtume, mkweli zaidi kuliko Allah Mtukufu, Aliye Mjuzi, Aliye Mtambuzi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net