Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 13

Faatir 35:13

فاطر

يُولِجُ ٱلَّيْلَ فِى ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِى ٱلَّيْلِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِى لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ لَهُ ٱلْمُلْكُ ۚ وَٱلَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ

Maana

Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia, kila kimoja kinakwenda kwa muda maalumu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Na hao mnaowaomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia. Kila kimojapo kinakwenda kwa muda maalumu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende. [13]

[13] Yeye huuingiza usiku katika mchana, na mchana katika usiku. Matokeo yake ni kuwa saa zao hurefuka na hufupika kwa mujibu wa mipango ya hikima miaka nenda miaka rudi. Na Yeye amelifanya jua na mwezi kutumika kwa manufaa yenu. Kila kimojapo kinakwenda kwa muda maalumu utao ishia kwake. Huyo mwenye shani kuu ndiye Mwenyezi Mungu Mwenye kuyapanga mambo yenu. Ufalme ni wake Yeye peke yake. Na hao wengineo mnao waomba kuwa ni miungu mnao waabudu hawawezi kumiliki hata ugozi mwembamba ule wa kokwa ya tende. Basi inakuwaje wastahili kuabudiwa? Aya hii tukufu inaonyesha kuwa jua lina muda utakao kwisha baadae. Na huenda kuwa huo ndio utao kuwa Mwisho kwa mujibu wasemavyo wataalamu wa ilimu ya Falaki (Astronomy) kwamba jua linaunguza kuni zake za Dharra (Nuclear fuel) nayo ni Hydrogen inayo geuka kuwa Helium. Huenda kuwa ukisha muda wa jua ndio Msiba Mkuu wa Ulimwengu wote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Anazitia nyakati za usiku ndani ya mchana, hivyo basi mchana ukarefuka kwa kadiri ya usiku unavyopungua; na Anazitia nyakati za mchana ndani ya usiku, hivyo basi usiku ukarefuka kwa kadiri ya mchana unavyopungua. Na Amedhalilisha jua na mwezi vikawa vinatembea kwa wakati maalumu. Huyo aliyefanya hili ndiye Allah Mtukufu Mola wenu. Ni Wake Yeye ufalme wote. Na wale mnaowaabudu badala ya Allah Mtukufu hawamiliki hata utandu mwembamba unaozunguka koko ya tende.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net