Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 52

Saba 34:52

سبإ

وَقَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِهِۦ وَأَنَّىٰ لَهُمُ ٱلتَّنَاوُشُ مِن مَّكَانٍۭ بَعِيدٍ

Maana

Na watasema: "Tunaiamini!" Lakini wataipata wapi kutoka huko mahali mbali?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na watasema: Tunaiamini! Lakini wataipata wapi kutoka huko mahala mbali? [52]

[52] Na watasema, watapo iona adhabu: Tunaiamini Haki! Na vipi wao waipate Imani kwa wepesi huo kutoka pahala mbali na dunia ambayo wakati wake umekwisha pita?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakanushaji watasema watakapoiona adhabu huko Akhera, «Tumemuamini Allah Mtukufu, Vitabu Vyake na Mitume Wake. Vipi wao waipate Imani na hali ni kwamba kuifikia kwao hiyo Imani ni kutoka mahali mbali?» kushawekwa kizuizi baina yao na hiyo, kwani mahali pake ni ulimwenguni, na huko walikanusha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net