Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 51

Saba 34:51

سبإ

وَلَوْ تَرَىٰٓ إِذْ فَزِعُوا۟ فَلَا فَوْتَ وَأُخِذُوا۟ مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ

Maana

Na lau ungeliona watakapobabaika, basi hapana pa kukimbilia! Na watakamatwa mahala pa karibu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau ungeli ona watapo babaika, basi hapana pa kukimbilia! Na watakamatwa mahala pa karibu. [51]

[51] Na lau kuwa utaona, ewe mwenye kuona, pale watapo fazaika makafiri kweli itapo dhihiri, basi hawatakuwa na pa kukimbilia. Na watachukuliwa wapelekwe kwenye Moto kutoka pahala karibu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau ungeona, ewe Mtume, pindi watakapobabaika wakanushaji pale watakapoishuhudia adhabu ya Allah Mtukufu, ungeona jambo kubwa! Hawatakuwa na uokozi wala makimbilio na watachukuliwa hadi Motoni kutoka mahali karibu pa kutwaliwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net