As-Sajda 32:6
السجدةذَٰلِكَ عَـٰلِمُ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyoonekana na yanayoonekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyo onekana na yanayo onekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. [6]
[6] Huyo ndiye aliye sifika kwa kuumba na kutawala na kupanga, Mwenye kuyajua ya ghaibu ya viumbe vyote na wanayo yaona, ambaye amri yake ni yenye kushinda, Mkunjufu wa rehema,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Huyo Muumbaji Mwenye kuendesha mambo ya viumbe ni Mjuzi wa kila kilichofichika kwenye macho, miongoni mwa mambo yanayohifadhiwa na vifua na kufichwa na nafsi, na ni Mjuzi wa vitu vinavyoonekana na macho, na Yeye Ndiye Mwenye nguvu, Ndiye Mwenye kushinda Asiyeshindwa, Ndiye Mwenye kuwarehemu waja Wake Waumini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net