Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 5

As-Sajda 32:5

السجدة

يُدَبِّرُ ٱلْأَمْرَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ إِلَى ٱلْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِى يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُۥٓ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ

Maana

Anapitisha mambo yote yaliyo baina ya mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyohesabu nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Anapitisha mambo yote yalio baina mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyo hisabu nyinyi. [5]

[5] Yeye huyaendesha mambo ya uumbaji katika mbingu na ardhi, kisha amri yake hupanda kwenda kwake kwa siku ambayo kadiri yake ni kama miaka elfu kwa mujibu wa miaka ya duniani mnayo ihisabu nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anaendesha mambo ya viumbe kutoka mbinguni hadi ardhini, kisha mambo hayo yanapanda kwa Allah Mtukufu kwa kipindi cha siku moja ambayo kadiri yake ni miaka elfu moja ya siku za duniani mnazozihesabu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net